Monday, February 10, 2014

INASEMEKANA ETI JESHI LA AUSTRALIA LAKAMATA MADAWA YA KULEVYA PWANI YA TANZANIA

Askari wa  HMAS Melbourne wakiwa na madawa yaliyokamatwa.
 Madawa hayo yakiharibiwa.
JESHI la majini la Australia limekamata na kuharibu kilo 353 za madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni 700 katika pwani ya Tanzania.
Askari wa meli ya HMAS Melbourne waliyagundua madawa hayo katika meli moja Jumatano iliyopita wakiwa katika shughuli za kupiga vita ugaidi na kuimarisha usalama maeneo ya  baharini Mashariki ya Kati na Bahari ya Hindi.
Mkuu wa kikosi hicho, Daryl Bates, alisema hatua hiyo ilikuwa ni pigo katika kukwamisha njia za kupatikana kwa fedha zinazotumiwa na magaidi.
Credits: AFP

No comments:

Post a Comment