Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za
kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa za kuongeza nguvu
hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa katika jamii
Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia
dawa hizo kama tiba ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao.
Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi
katika jamii yetu.
Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba
wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile za
hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa kuwa
watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie ‘kolezo’ la
kuwasaidia kuamsha hisia zao.
Kwa wanaume, ukosefu wa nguvu ni jambo
linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao wako tayari
kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la
ndoa ikuwa katika miliki yao daima.
Lakini, watafiti wa masuala ya mapenzi
nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika
kupungukiwa nguvu za kiume, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna
wanavyoweza kuepukana na kasoro hizo.
Ushahidi uliopatikana kwa waathirika wa
tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili upungufu wa nguvu za
kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama upande wa
pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.
Zipo kesi za wanaume kujiua au
kujinyofoa sehemu zao za siri kwa sababu ya kushindwa katika tendo la
ndoa. Hali hii inatoa picha kwamba wanaume wengi hujitwika mzigo wa
lawama wenyewe.
Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo
Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa
kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami
nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:
1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume
hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa
HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya
tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia
ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke
anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali
ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume
zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani
siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”
2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye
ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia
mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya
mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake
mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa
vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini
wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha
kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi
wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza
uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo
kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa
na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe
kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi,
asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi,
hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na
kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza
kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote
tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa
tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume
apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na
mwili ni muhimu sana katika mapenzi.
GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia
mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya
uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi,
usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha tatizo
la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya
kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda
kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa
wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa
wanawake wa nje kuliko wake zao hao.
USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo
kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana
moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi
ambayo humuondolea hamu ya tendo.
No comments:
Post a Comment