You Heard: Khalid Chokoraa akamatwa na noti Bandia
Mwanamuziki Khalid Chokoraa, akutwa na pesa bandia feri alipokuwa akijaribu kuvuka kurudi mjini baada ya kutoka Kigamboni.
kwa mujibu wa mtu aliekuwepo kwaribu amesema, Chokoraa alikuwa akinunua tickets kwa ajili ya kuvuka katika kivuko cha kigamboni ila baada ya kutoa noti ya shilingi 10,000 dada aliekua akikata ticket alishtuka na kuona ni noti bandia na kumuitia polisi wakamdaka na kumshikilia kwa takribani dakika 45.
Inasemekana Chokoraa hakuwa peke yake, bali alikuwa na akina dada watatu ambao wote walipigwa sachi na maaskari kujua kama wana pesa zingine za bandia, lakini kwa bahati hawakuwa na pesa zingine zozote chafu au salama na baadae kuachiwa
msikilize Chokoraa mwenyewe hapa chini .
at 2:14 PM
No comments:
Post a Comment