Monday, August 25, 2014
KUHUSU DANCER WA NICKI MINAJ KUGONGWA NA NYOKA
Dancer wa Nicki Minaj ang'atwa na nyoka aina ya anaconda wakati wa mazoezi ya kucheza wimbo wa 'Anaconda'
posted 1 day ago by admin
Mmoja kati ya wachezaji wa Nicki Minaj ameng’atwa na nyoka aina ya Anaconda mwenye urefu wa futi 6 wakati wakifanya mazoezi ya kwa ajili ya show ya tuzo za video za MTV (MTV Video Music Awards).
Kwa mujibu wa TMZ, Nicki Minaj alikuwa jukwaani na dancers wake wakifanya mazoezi ya kucheza hit ya ‘Anaconda’ ambapo dancer mmoja wa kike aling’atwa na moja kati ya nyoka waliokuwa wamewekwa kwenye kontena kwa ajili ya kufanyia mazoezi.
Inaelezwa kuwa nyoka hao aina ya Anaconda hawakuwa na sumu lakini wana uwezo wa kusambaza bacteria ambao husababisha matatizo kiafya.
Msichana huyo alipelekwa hospitalini kupata matibabu.
Haijulikani kama bado Nicki Minaj atapanda na nyoka hao katika jukwaa la MTV VMAs, Jumapili .
Nicki hatakuwa mwimbaji wa kwanza kupanda na nyoka kwenye tuzo hizo, mwaka 2001 Britney Spears alipanda na joka kubwa wakati anaimba ‘I’m A Slave 4 U’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment