Saturday, April 19, 2014

STORI KARI YA LEO KUHUSU POLISI HUYU

Jeshi la polisi Mbeya limemkamata  Askari polisi mwanamke wa Dar es salaam kwa tuhuma za kumuiba mtoto  mchanga wa siku ambae aliibwa toka April 6 2014 kwa kushirikiana na baba mzazi.
Ahmed Msangi ambae ni kamanda wa polisi Mbeya amesema ‘tulimkamata huyu Mama na mtoto na hivi sasa Mwanamke huyu yuko mahabusu pamoja na baba mtu, tulichofanya niliagiza OCD wa Kyela amlete mama halisi wa mtoto ili aungane na mwanae na vilevile kukamilisha upelelezi, Mwanamke huyu anaitwa Prisca askari Polisi Tabata mwenye namba WP5367′

‘Sasa hivi yuko chini ya ulinzi, huu ni uhalifu kwa sababu ni wizi wa mtoto… nimeshaagiza mashtaka ya kijeshi na yanaendelea na tukishajiridhisha hatua stahiki za kitendo alichofanya zichukuliwe, ukifanya uhalifu adhabu yake ni kufukuzwa kazi ili tukupeleke Mahakamani ukashtakiwe, amefanya kitendo kibaya kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la Polisi, kila mtu atachukua mzigo wake mwenyewe’

Kamanda wa polisi amesema Baba wa mtoto na askari huyo hawana uhusiano wa damu bali wa kibiashara hivyo wanaendelea na uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment