ANGALIA PICHA KIJANA NUSURA KUFA BAADA YA KUIBA NGURUWE UKO MOSHI
KATIKA kuelekea sikuu za Krismasi na Mwaka mpya pilika pilika
zimeongezeka katika mji wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla huku
vibaka pia wakiendelea na udokozi na wizi wa vitu mbalimbali.
Katika kuthibitisha hilo juzi Tanzania Daima limeshuhudia mkazi wa
kijiji cha Nshara, Machame wilayani Hai,ambaye jina lake halikupatikana
mara moja amenusurika kuuawa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi wenye
hasira kumshambulia kwa silaha za jadi baada ya kuiba kitoto cha nguruwe
maarufu kama "Kiti moto".
Tukio hilo la aina yake ambalo linaashiria maandalizi ya siku kuu hizo
lilitokea juzi majira saa 5.30 asubuhi kijijini humo baada ya mkazi huyo
kuonekana akiwa amembeba mnyamya huyo begani akiwa katika mfuko,maarufu
kama Sandarusi mithili ya mzigo wa kawaida.
Akizungumzia tukio hilo,mkazi wa kijiji cha Nshara, Husein Mbaruku
alisema mtu huyo alionekana akinyata katika banda la Nguruwe akiwa na
mfuko wake akiamini kuwa hakuna mtu aliyemuona ingawa wenyeji nao
walikuwa wakimvizia ili kuona anachotaka kufanya.
"Huyu bwana ni mwizi mzoefu katika eneo hili ,mara
kwa mara wenyeji hapa wamekuwa wakilalamika kuibiwa nguruwe wao leo
naona Arobaini yake imefika ,wananchi wamemkamata na ndio hivyo kama
unavyoona kapigwa sana"alisema Mbaruku.
Alisema mtu huyo alifanikiwa kuiingia katika banda la nguruwe na
kukikamata mmoja ya kitoto cha nguruwe ambacho wakati wa harakati ya
kuingizwa katika mfuko huo kilipiga kelele ambazo ziliwashitua majirani
wengine.
Kutokana na mazingira hayo,mtuhumiwa huyo alikuwa mjasiri na kukimbia
nacho hivyo hivyo jambo lililosababisha baadhi ya wananchi kuanza
kumfukuza kwa kasi ndipo alipoanguka eneo la mfoni ambapo wananchi
walimjeruhi kwa silaha hizo ikiwamo mawe.
Katika hali isiyo ya kawaida huku mtuhumiwa huyo akivuja damu nyingine
mmoja wa raia alitaka kumchoma kwa gurudumu la gari ndipo wananchi
wenzake walipoingilia kati na kumuokoa mtuhumuwa huyo ambaye alipelekwa
kituo cha polisi bomangombe.
Hadi kipindi hiki kinaondoka eneo la tukio majira ya saa saba mchana
mtuhumiwa huyo alikuwa hajitambui kutokana na kipigo hicho kutoka kwa
raia ambao baadaye walitawanyika baada ya kuhisi wamefanya mauaji.
Mkazi wa kijiji cha Nshara Machame akivuja damu baada ya kupokea kipigo
kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kufuatia wizi wa mtoto wa
Nguruwe,tukio hilo lilitokea juzi wilayani Hai.Picha na Dixon Busagaga
wa
"Huyu bwana ni mwizi mzoefu katika eneo hili ,mara kwa mara wenyeji hapa wamekuwa wakilalamika kuibiwa nguruwe wao leo naona Arobaini yake imefika ,wananchi wamemkamata na ndio hivyo kama unavyoona kapigwa sana"alisema Mbaruku.
No comments:
Post a Comment