Jokate na Wema historia
yao ilianzia kwenye shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006 ambapo
Mshindi alikua ni Wema Sepetu akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu
akiwa Lissa Jensen.
Vichwa vya habari vilikuja kutengenezwa tena vikiwahusisha warembo hawa kuonekana wako na
mtu mmoja ambapo magazeti na mitandao mingi iliandika mahusiano haya yaliyokua
yakimhusu Diamond Platnumz kutoka na warembo hawa.
Kimepita
kimya kirefu sana juu ya hawa watu wawili hadi usiku wa February 01
huko Arusha kwenye Tamasha la Divaz Night Endless Fame ambalo ndani yake
kulikua na mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Aunt Ezekiel,Martin
Kadinda,Kajala,Zamaradi Mketema,Chid Benzi,Mirror,Jordan na wengine
kibao.
Wakati
Madam Wema Sepetu akimwaga mauno kwenye jukwaa bila kutegemewa na mtu
yoyote Jokate alipanda Jukwaani na kuanza kumtunza Wema pesa na wakati
huo Wema alikua akicheza Wimbo wa Diamond My Number One ‘Ngololo’ ambapo
Jokate aliungana na Wema kuucheza Wimbo huo.
No comments:
Post a Comment